Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Warsha maalumu na ya kiutendaji yenye mada “Vigezo, Mifano na Mchakato wa Nadharia za Kimataifa” ikiangazia Tuzo ya Kimataifa ya Shahidi Sadr, itafanyika siku ya Jumapili, tarehe 13 Mehr 1404 (saa 2:00–5:00 asubuhi) katika jengo la maktaba, Kitengo cha Utafiti cha Jame’atuz-Zahra (s).
Warsha hii itafundishwa na Hujjatul-Islam wal-Muslimin Dkt. Yahya Jahangiri kwa lengo la kuwawezesha watafiti, wanafunzi wa ngazi ya tatu, ngazi ya nne na wale wa fiqhi ya juu katika uwanja wa nadharia za kimataifa.
Muda wa mwisho wa kujisajili katika warsha hii umewekwa hadi tarehe 12 Mehr 1404, na wanaopenda kushiriki wanaweza kujisajili kupitia anuani ya mtandaoni: forms.jz.ac.ir/f_25.
Your Comment